Jumatano 25 Februari 2026 - 11:10
Ujumbe wa "Jumuiya ya wanazuoni Lebanon" uliohudhuria katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa “Machweo ya Jua” kwenye kaburi la shahidi Nasrullah

Hawza/ Ujumbe kutoka kwa "Jumuiya ya wanazuoni Lebanon", ulishiriki katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza ya “Machweo ya Jua” iliyofanyika katika kaburi tukufu la Bwana wa Mashahidi wa Umma, Hassan Nasrullah.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, "Jumuiya ya wanazuoni Lebanon", katika taarifa yake ilitangaza kwamba, ujumbe kutoka taasisi hiyo ulishiriki katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza ya “Machweo ya Jua” iliyofanyika katika kaburi tukufu la Bwana wa Mashahidi wa Umma, Sayyid Hassan Nasrullah.

Ujumbe huo ulimhusisha Sheikh Hussein Ghabris (mkuu wa mahusiano ya umma), Sheikh Maher Mazhar (mkuu wa mahusiano ya nje) na Sheikh Muhammad Al-Lababidi (mjumbe wa Baraza Kuu).

Katika hafla hiyo, kundi la mujahidina wanaohusishwa na Jeshi la Uhamasishaji wa Umma la Wanyonge na Vikosi vya Muqawama vya Lebanon waliapa kiapo cha jihadi na uaminifu, na wakahuisha ahadi yao ya kuendeleza njia ya Muqawama wa Kiislamu na kushikamana na mstari wake halisi wa kijihadi.

Mwisho, ujumbe wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu uliweka shada la maua juu ya kaburi tukufu, na wajumbe wake wakasoma Suratul-Fatiha.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha